Lugha ya Kiswahili
Mtandao huu unatoa maelezo, tanzu na vipengee vya Lugha ya Kiswahili. Maelezo hata yanalenga kumuelimisha msomaji kwa ufususi ili aweze kuijua lugha hii. Mtandao huu unatumia maelezo huru ambayo hayajanukuliwa kutoka makala yoyote. Hisia za mtandao huu ni Mali ya mwandishi binafsi na zinaweza kubadilishwa panapo uamuzi wa mwandishi. Msomaji ana kila gaki kunukuu chochote bila kuubadilisha ujumbe.
Monday, 11 July 2016
Sunday, 10 July 2016
Kiswahili na changamoto zake nchini Kenya
Kiswahili ni Lugha ya kwanza ya jamii ya Waswahili wanaopatikana kusini mashariki kwa Afrika. Kiswahili pia ni lugha rasmi katika nchi ya Kenya na Tanzania. Hutumika pia katika nchi zingine kama Sudan Kusini, Uganda, Zaire, Visiwa vya Comoro kati ya zinginezo. Zaidi ya watu millioni arobaini huzungumza Kiswahili kama lugha yao ya kwanza.
Nchini Kenya, lugha hii imezidi kukua kwa kasi. Lugha hii ni some rasmi linalotahiniwa katika mitihani ya kitaifa. Zaidi ya vituo vya redio 15 hutoa matangazo kwa Lugha hii ya Kiswahili. Mifano ni Citizen, Radio Maisha, Milele Fm, Baraka FM na kadhalika. Pia makala ya gazeti kama Taifa Leo hutumia Kiswahili.
Rais huhutubia wananchi kwa Kiswahili katika hadhara za kitaifa kila anapotoa hotuba.
Lugha hii hukumba changamoto kama;
1. Kuwepo kwa kiingereza kama Lugha rasmi.
2. Kuwepo kwa lugha ya vijana, sheng, ambayo haizingatii kanuni za lugha.
3. Ukosefu wa hamu ya kusoma Kiswahili.
4. Ukosefu wa wakufunzi wa Kiswahili.
5.

Nomino za kiswahili
Nomino ni neno linalotaja kitu, Mtu, mahali au hisia. Zifuatazo ni aina za nomino zinazokubalika katika lugha ya kiswahili:
1. NOMINO ZA VIKUNDI AU JAMII
Majina ya vitu vinavyopatikana kwa wingi au makundi. Mifano msafara wa magari, thurea la nyota, umati wa watu, darasa la wanafunzi, na kadhalika.
2. NOMINO ZA DHAHANIA
Nomino hizi hazigusiki, hazionekani na hazihesabiki. Mifano ni furaha, hasira, elimu, hisia, na kadhalika.
3. NOMINO ZA KAWAIDA
Haya ni majina yanayotumiwa kurejelea vitu vya kawaida kama watu, nyumba, mimea, nyumba,kitu, na kadhalika. Nomino hizi hubadilika katika hali ya umoja na wingi kwa kutegemea ngeli.
4. NOMINO ZA KIPEKEE
Ni majina spesheli yanayotumika kutambua nomino za kawaida kwa ubinafsi. Mifano ni majina ya kampuni, shule, watu, nchi, milima, miji na kadhalika. Mifano Arasa, Kenya, Nile, Kisii, Facebook, na kadhalika. Herufi ya kwanza huanza na herufi kubwa.
5.NOMINO ZA WINGI
Ni majina ya vitu visivyohesabika lakini vinagusika. Mfano sukari, chumvi, nywele, maji na maziwa.
6. NOMINO ZA KITENZI JINA
ni nomino zinazoundwa kutokana na vitenzi. Majina hata huundwa kwa kuongeza KU nyuma ya mzizi wa kitenzi. Mifano kucheza, kusoma, kulala, kuruka na kadhalika.

Subscribe to:
Posts (Atom)