Kiswahili ni Lugha ya kwanza ya jamii ya Waswahili wanaopatikana kusini mashariki kwa Afrika. Kiswahili pia ni lugha rasmi katika nchi ya Kenya na Tanzania. Hutumika pia katika nchi zingine kama Sudan Kusini, Uganda, Zaire, Visiwa vya Comoro kati ya zinginezo. Zaidi ya watu millioni arobaini huzungumza Kiswahili kama lugha yao ya kwanza.
Nchini Kenya, lugha hii imezidi kukua kwa kasi. Lugha hii ni some rasmi linalotahiniwa katika mitihani ya kitaifa. Zaidi ya vituo vya redio 15 hutoa matangazo kwa Lugha hii ya Kiswahili. Mifano ni Citizen, Radio Maisha, Milele Fm, Baraka FM na kadhalika. Pia makala ya gazeti kama Taifa Leo hutumia Kiswahili.
Rais huhutubia wananchi kwa Kiswahili katika hadhara za kitaifa kila anapotoa hotuba.
Lugha hii hukumba changamoto kama;
1. Kuwepo kwa kiingereza kama Lugha rasmi.
2. Kuwepo kwa lugha ya vijana, sheng, ambayo haizingatii kanuni za lugha.
3. Ukosefu wa hamu ya kusoma Kiswahili.
4. Ukosefu wa wakufunzi wa Kiswahili.
5.
No comments:
Post a Comment