Sunday, 10 July 2016

Nomino za kiswahili

Nomino ni neno linalotaja kitu, Mtu, mahali au hisia. Zifuatazo ni aina za nomino zinazokubalika katika lugha ya kiswahili:

1. NOMINO ZA VIKUNDI AU JAMII
Majina ya vitu vinavyopatikana kwa wingi au makundi. Mifano msafara wa magari, thurea la nyota, umati wa watu, darasa la wanafunzi, na kadhalika.
2. NOMINO ZA DHAHANIA
Nomino hizi hazigusiki, hazionekani na hazihesabiki. Mifano ni furaha, hasira, elimu, hisia, na kadhalika.

3. NOMINO ZA KAWAIDA
Haya ni majina yanayotumiwa kurejelea vitu vya kawaida kama watu, nyumba, mimea, nyumba,kitu, na kadhalika. Nomino hizi hubadilika katika hali ya umoja na wingi kwa kutegemea ngeli.

4. NOMINO ZA KIPEKEE
Ni majina spesheli yanayotumika kutambua nomino za kawaida kwa ubinafsi. Mifano ni majina ya kampuni, shule, watu, nchi, milima, miji na kadhalika. Mifano Arasa, Kenya, Nile, Kisii, Facebook, na kadhalika. Herufi ya kwanza huanza na herufi kubwa.

5.NOMINO ZA WINGI
Ni majina ya vitu visivyohesabika lakini vinagusika. Mfano sukari, chumvi, nywele, maji na maziwa.

6. NOMINO ZA KITENZI JINA
ni nomino zinazoundwa kutokana na vitenzi. Majina hata huundwa kwa kuongeza KU nyuma ya mzizi wa kitenzi. Mifano kucheza, kusoma, kulala, kuruka na kadhalika.



5 comments: